19
December
2016
KAMPUNI YA ELITE ORGANIZING SERVICES YATOA MSAADA WA PAD KWA WANAWAKE WA MABWEPANDE
Zikiwa zimepita siku 96 tangu kuzindua kampeni ya Declutter&Donate ambayo ina lengo la kuwasaidia watoto wenye mahitaji na wanawake ambao wanaishi Mabwepande, Dar, hatimaye kampuni ya Elite Organizing Services Limited imekamilisha ahadi ya kuwapa msaada wa taulo za hedhi wanawake wa Mabwepande pamoja na kuwapa elimu kuhusu hedhi salama. Akizungumza kuhusu msaada huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo alisema wameona ni vyema kuanza na wanawake wa Mabwepande kutokana na changamoto ambazo zinawakabili kwani lengo lao ni kuwasaidia wanawake ambao wanaishi katika mazingira magumu.
19
December
2016
Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo aki
“Kampeni ya Declutter&Donate ndiyo imefanyika kwa mara ya kwanza na sehemu ya kwanza tulichagua Mabwepande, tumechagua hapa sababu wakazi wa hapa waliathirika na mafuriko ya mwaka 2012, huu ni mji mpya na una changamoto zake, serikali inafanya kwa nafasi yake na wananchi kwa sehemu yake, sisi tunafanya kazi sehemu ya wananchi kupunguza changamoto za wakazi wa Mabwepande, “Lengo letu ni kufika sehemu zote ambazo zina mazingira magumu kwa mwanawake lakini inabidi kuanza taratibu ili kuona kile unachokifikiria ni kweli kinaleta mabadiliko kwa jamii, na tumeona tuanze Mabwepande tulete semina na tuone manufaa yake na vile vitu ambavyo havikuleta mabadiliko chanya turekebishe ili tusogee kwenda sehemu nyingine na lengo kufika sehemu yoyote Tanzania,” alisema.
19
December
2016
Mfaidika wa msaada wa Declutter&Donate, Rhoda Mwinami akielezea jinsi ambavyo wameelimika kutokana na elimu ya hedhi salama wali
Nae mmoja wa wafaidika na msaada Rhoda Mwinami alisema elimu ambayo wamepatiwa imewasaidia kufahamu mambo ambayo hawakuwa wakifahamu awali kuhusu hedhi na hivyo itawasaidia kujitunza na kuwa wasafi hali ambayo itawapunguzia hata baadhi ya magonjwa yanayotokana na usafi katika kipindi cha hedhi. “Tumejifunza jinsi ya kujitunza na hedhi salama … kabla ya kupata elimu tulikuwa tunajua tukiingia unatumia kitambaa au kutumia pad lakini jinsi ya kufanya usafi mara ngapi tulikuwa hatujui lakini sasa hivi tumejua jinsi ya kufanya, nimepanga takuwa nakutana na mabinti na kuwaeleza jinsi gani wanatakiwa kujitunza,” alisema Rhoda.
19
December
2016
Mwenyekiti wa mtaa wa Mji Mpya uliopo kata ya Mabwepande, Justin Chiganga akizungumza na wananchi wake kuhusu ahadi ya kampuni y
19
December
2016
Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo aki
19
December
2016
Timu ya Declutter&Donate ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanufaika wa elimu ya hedhi salama na msaada wa taulo za hedh
18
September
2016
NASRA MBULULO : Ajipanga kuwasaidia waliopo mtaani
Kwa ufupi anasema wazo la kuanzisha kampeni hiyo lilikuja baada ya Rais John Magufuli kutangaza kwamba siku ya maadhimisho ya Uhuru itasherekewa kwa nchi kufanya usafi katika maeneo yanayotuzunguka ili kuepuka magonjwa mbalimbali ikiwamo kipindupindu.
13
September
2016
KAMPENI YA DECLUTTER&DONATE YAANZA KUFANYIKA DAR, LENGO LA KUSAIDIA WANAWAKE NA WATOTO
Kwa kutambua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wanawake wanaoishi katika mazingira magumu kampuni ya Elite Organizing Services Limited Septemba, 13 ya mwaka huu ilifanya uzinduzi wa Kampeni ya Declutter&Donate ambayo ina lengo la kusaidia wanawake na watoto, sasa kampeni hiyo imeanza kufanyika jijini Dar es Salaam. Akizungumzia siku ya kwanza ya kampeni hiyo ambayo inaendeshwa kwa kukusanya vitu mbalimbali vya nyumbani na maofisini ambavyo vinakuwa havitumiki, Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo alisema mapokeo ya kampeni hiyo hayajawa makubwa lakini kwa wachache ambao wamejitokeza wameweza kuchangia vitu ambavyo wanakusudia kuvikusanya.
13
September
2016
Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo
“Tunachukua vifaa vya michezo, midoli, vitabu, samani za nyumbani na ofisini, tv, redio deki na vitu vingine visivyotumika na mwamko umekuwa mdogo lakini kwa waliojitokeza wametoa vitu vizuri ambavyo tumekuwa tukivitaka, siku ya kwanza imekuwa na watu wachache lakini imekuwa siku nzuri kwa kukusanya tunachohitaji, “Kampeni hii imeanzishwa ikiwa na malengo ya kusaidia wanawake ambao wanaishi katika mazingira magumu na watoto, na leo ni siku ya kwanza lakini tunataraji kwenda kufanya na sehemu nyingi ili kukusanya na baadae tukawasaidie watu ambao tumewakusudia,” alisema Nasra.
13
September
2016
Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo
Alisema baada ya zoezi hilo kuendeshwa katika Shule ya Sekondari Tambaza, wanataraji kulifanya tena Oktoba, 16 katika Shule ya Msingi Oysterbay, na baada ya hapo watatangaza sehemu nyingine ambazo zitafuatia. Alisema kuwa baada ya zoezi la ukusanyaji kumalizika watakwenda kutoa semina inayohusu afya kwa wanawake wanaoishi Mabwepande na kisha kwenda katika kituo cha kulelea watoto kwa ajili ya kuwapatia msaada ambao umepatikana kutokana na zoezi ambalo wanalifanya sasa la kukusanya vitu ambavyo havitumiwi majumbani na maofisini.
13
September
2016
Mkurugenzi wa Kampuni ya Elite Organizing Services Limited na mwanzilishi wa kampeni ya Declutter&Donate, Nasra Karl Mbululo na
“Disemba, 15 tutatoa semina ya afya ya mwanamke na hedhi salama na watapata nafasi ya kufanyiwa uchunguzi na kuzungumza na madaktari kisha tutawapatia taulo za hedhi (pad), tumekadiria ziwe za miezi sita, “Baada ya hapo, Disemba, 20 tutakwenda kutoa msaada kwa kituo cha watoto ambacho tutakitaja hapo baadae kwahiyo niwaombe watu ambao wana vitu ambavyo sisi tunavihitaji watupatie ili vitumike kuwasaidia wengine,” alisema Nasra.
13
September
2016
KAMPUNI YA ELITE KUTOA MISAADA KWA WANAWAKE WAISHIO MABWEPANDE
Kutokana na hali ya kimaisha kwa wananchi ambao wanaishi eneo la Mabwepande, Kampuni ya Elite Organizers Service imefanya uzinduzi wa kampeni ya Declutter&Donate ambayo inalenga kuwasaidia wanawake wanaoishi eneo hilo ili kuwapatia msaada wa taulo za hedhi (pad). Akizungumzia kampeni ya Declutter&Donate ambayo imezinduliwa Jumanne ya Septemba, 13, Mwanzilishi wa kampuni ya Elite Organizers Service, Nasra Karl Mbululo alisema kuwa kampeni hiyo imezinduliwa mahsusi kwa ajili ya kuwasaidia wanawake na watoto yatima. Alisema kampeni hiyo itahusika na kukusanya vitu ambavyo havitumiki nyumbani na maofisini na kisha vitauzwa na baadae watakwenda kutoa taulo za hedhi kwa wanawake 814 ambao wanaishi eneo la Mabwepande. Kwa upande wa watoto yatima, Nasra alisema kuwa watakusanya vitabu na midoli kutoka kwa watu mbalimbali ambao watakuwa tayari kujitolea na baadae watapeleka katika moja ya kituo ambacho watakichagua.
13
September
2016
Mwanzilishi wa kampuni ya Elite Organizers Service, Nasra Karl Mbululo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya Decl
Kutokana na hali ya kimaisha kwa wananchi ambao wanaishi eneo la Mabwepande, Kampuni ya Elite Organizers Service imefanya uzinduzi wa kampeni ya Declutter&Donate ambayo inalenga kuwasaidia wanawake wanaoishi eneo hilo ili kuwapatia msaada wa taulo za hedhi (pad). Akizungumzia kampeni ya Declutter&Donate ambayo imezinduliwa Jumanne ya Septemba, 13, Mwanzilishi wa kampuni ya Elite Organizers Service, Nasra Karl Mbululo alisema kuwa kampeni hiyo imezinduliwa mahsusi kwa ajili ya kuwasaidia wanawake na watoto yatima. Alisema kampeni hiyo itahusika na kukusanya vitu ambavyo havitumiki nyumbani na maofisini na kisha vitauzwa na baadae watakwenda kutoa taulo za hedhi kwa wanawake 814 ambao wanaishi eneo la Mabwepande. Kwa upande wa watoto yatima, Nasra alisema kuwa watakusanya vitabu na midoli kutoka kwa watu mbalimbali ambao watakuwa tayari kujitolea na baadae watapeleka katika moja ya kituo ambacho watakichagua.
05
March
2016
Plan, Organize & Succeed
An exclusive event for network marketers who needed guidance and motivation to grow their business as a group. We discuss challenges they face on setting up their goals and how to overcome them.
28
February
2016
Special kwa Mwanamke:Jinsi ya kupangilia vipaumbele vyako

Feda Events wametuandalia event hii muhimu kwetu wanawake wote wa jiji la Dar es salaam, ambapo lengo lao kuu ni kutusaidia wanawake tuweze  kufanya mambo kwa kufuata malengo tunayojiwekea na kwa muda mahususi

Kupitia Event hii, Wanawake tutajifunza

  1. Jinsi ya Kupanga malengo yetu
  2. Namna ya Kuyapa kipaumbele  malengo tuliyojiwekea na
  3. Vitu ambavyo tunaweza fanya kila siku ili kutimiza malengo yetu
  4. Namna nzuri ya Upangaji wa nyumba zetu, itakayofanya nyumba kuwa na muonekano mzuri,kuokoa muda na kuondoa msongo wa mawazo

Msemaji mkuu katika event hii ni Nasra Karl ambaye ni Professional organizer for business and homes

Atakuwepo na Khale Fatma “Manjano Dream Maker 2016” ambaye atazungumzia umuhimu na namna ya kuchagua vipodozi sahihi kwa ngozi zetu na pia atafanya make up skin  testing kwa wanawake wote tutakao taka jua ni make up gani inafaa kwa ngozi zetu

Pia tutakuwa na Gonzaga Rugambwa ,Mwanzilishi wa klabu ya wasoma vitabu wa Dar es salaam, Darbook Club ambaye atazungumzia namna tabia ya usomaji vitabu inavyoweza boresha maisha yetu kama wanawake na kugusia pia umuhimu wa kutunza kumbukumbu za fedha kwa mwanamke.

Ni Jumapili tarehe 28 mwezi huu wa pili, pale Upanga club, kuanzia saa tisa hadi kumi na moja na nusu jioni, Kwa kiingilio cha 15,000/= tu, kwa mawasiliano na kufanya booking mapema piga 0712015429 au waweza tuma email kwa felistad@gmail.com